Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 3:56-65 Biblia Habari Njema (BHN)

56. Wewe umenisikia nikikulilia:‘Usiache kusikia kilio changu cha msaadabali unipatie nafuu.’

57. Nilipokuita ulinijia karibuukaniambia, ‘Usiogope!’

58. “Umenitetea katika kisa changu ee Mwenyezi-Mungu,umeyakomboa maisha yangu.

59. Umeuona uovu niliotendewa ee Mwenyezi-Mungu,uniamulie kwa wema kisa changu.

60. Umeuona uovu wa maadui zangu,na mipango yao yote ya hila dhidi yangu.

61. “Umesikia matukano yao ee Mwenyezi-Mungu,na mipango yao yote ya hila dhidi yangu.

62. Maneno na mawazo ya maadui zangu siku nzimani juu ya kuniangamiza mimi.

63. Wakati wote, wamekaa au wanakwenda,mimi ndiye wanayemzomea.

64. Uwalipize, ee Mwenyezi-Mungukadiri ya hayo matendo yao,kadiri ya mambo waliyotenda wenyewe.

65. Uipumbaze mioyo yao,na laana yako iwashukie.

Kusoma sura kamili Maombolezo 3