Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 3:47-53 Biblia Habari Njema (BHN)

47. Kitisho na hofu vimetuandama,tumepatwa na maafa na maangamizi.

48. Macho yangu yabubujika mito ya machozikwa sababu ya kuangamizwa kwa watu wangu.

49. “Machozi yatanitoka bila kikomo,

50. mpaka Mwenyezi-Mungu kutoka huko mbinguniaangalie chini na kuona.

51. Nalia na kujaa majonzi,kuona yaliyowapata kina mama wa mji wangu.

52. “Nimewindwa kama ndegena hao wanichukiao bila sababu.

53. Walinitupa shimoni nikiwa haina juu yangu wakarundika mawe.

Kusoma sura kamili Maombolezo 3