Agano la Kale

Agano Jipya

Maombolezo 3:37-45 Biblia Habari Njema (BHN)

37. Nani awezaye kuamuru kitu kifanyikeMwenyezi-Mungu asipopanga iwe hivyo?

38. Maafa na mema hutokea tukwa amri yake Mungu Mkuu.

39. Kwa nini mtu anung'unike,ikiwa ameadhibiwa kwa dhambi zake?

40. Na tupime na kuchunguza mwenendo wetu,tupate kumrudia Mwenyezi-Mungu.

41. Tumfungulie Mungu huko mbingunimioyo yetu na kumwomba:

42. “Sisi tulikukosea na kukuasinawe bado hujatusamehe.

43. “Umejizungushia hasira yako ukatufuatia,ukatuua bila huruma.

44. Umejizungushia wingu zito,sala yeyote isiweze kupenya humo.

45. Umetufanya kuwa takataka na uchafumiongoni mwa watu wa mataifa.

Kusoma sura kamili Maombolezo 3