16. Amenisagisha meno katika mawe,akanifanya nigaegae majivuni.
17. Moyo wangu haujui tena amani,kwangu furaha ni kitu kigeni.
18. Nimewaza “Nimekata tamaa kabisa,tumaini langu kwa Mwenyezi-Mungu limetoweka.”
19. Kukumbuka taabu na kutangatanga kwangukwanipa uchungu kama wa nyongo.
20. Nayafikiria hayo daima,nayo roho yangu imejaa majonzi.
21. Lakini nakumbuka jambo hili moja,nami ninalo tumaini:
22. Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi,huruma zake hazina mwisho.