Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 6:15-30 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Wana wa Simeoni walikuwa: Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli; huyu wa mwisho alikuwa mtoto wa mwanamke wa Kikanaani. Hao walikuwa mababu wa jamaa za Simeoni.

16. Sasa yafuata majina ya wana wa Lawi na wazawa wao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137.

17. Wana wa Gershoni walikuwa: Libni na Shimei; jamaa zao zilitajwa kwa majina yao.

18. Wana wa Kohathi walikuwa: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133.

19. Wana wa Merari walikuwa: Mahli na Mushi. Hao ndio mababu wa jamaa za Walawi.

20. Amramu alimwoa Yokebedi, shangazi yake, naye akamzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137.

21. Na watoto wa kiume wa Ishari walikuwa: Kora, Nefegi na Zikri.

22. Watoto wa kiume wa Uzieli walikuwa: Mishaeli, Elsafani na Sithri.

23. Aroni alimwoa Elisheba, binti yake Aminadabu, dada yake Nashoni; naye akamzalia Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

24. Nao watoto wa kiume wa Kora walikuwa: Asiri, Elkana na Abiasafu, ambao walikuwa mababu wa jamaa za Kora.

25. Eleazari, mwana wa Aroni, alimwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi. Hawa ndio waliokuwa wakuu wa jamaa za Lawi.

26. Aroni na Mose ndio walioambiwa na Mwenyezi-Mungu, “Watoeni watu wa Israeli kutoka nchi ya Misri, vikundi kwa vikundi.”

27. Ndio haohao Mose na Aroni walioongea na Farao, mfalme wa Misri, juu ya kuwatoa Waisraeli nchini Misri.

28. Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoongea na Mose nchini Misri,

29. alimwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. Mwambie Farao, mfalme wa Misri, maneno yote ninayokuambia.”

30. Lakini Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Mimi sina ufasaha wa kuongea; Farao atanisikilizaje?”

Kusoma sura kamili Kutoka 6