Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 40:9-17 Biblia Habari Njema (BHN)

9. “Kisha, utaliweka wakfu hema takatifu pamoja na vyombo vyake vyote kwa kuvipaka yale mafuta ya kupaka, nalo litakuwa takatifu.

10. Halafu, utaiweka wakfu madhabahu ya kuteketezea sadaka na vyombo vyake vyote kwa kuipaka mafuta, nayo itakuwa takatifu kabisa.

11. Birika la kutawadhia na tako lake pia utaliweka wakfu kwa namna hiyohiyo.

12. “Utamwita Aroni na wanawe waje mlangoni mwa hema la mkutano, kisha uwatawadhe.

13. Mvike Aroni yale mavazi matakatifu; utampaka mafuta na kumweka wakfu, ili aweze kunitumikia kama kuhani.

14. Waite wanawe na kuwavisha zile kanzu.

15. Kisha uwapake mafuta kama ulivyompaka baba yao, ili nao pia wanitumikie kama makuhani. Kupakwa mafuta huku kutawaingiza katika ukuhani wa kudumu katika vizazi vyao vyote.”

16. Basi, Mose alitekeleza kikamilifu kabisa maagizo yote ya Mwenyezi-Mungu.

17. Mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza mwaka wa pili baada ya kutoka Misri, hema la mkutano lilisimikwa.

Kusoma sura kamili Kutoka 40