Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 40:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,

2. “Mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, utalisimika hema takatifu la mkutano.

3. Ndani ya hema hilo utaweka lile sanduku la ushuhuda, kisha weka pazia mbele yake.

4. Utaiingiza meza na kupanga vyombo vyake juu. Utaingiza kile kinara pia na kuziweka taa zake juu yake.

5. Madhabahu ya dhahabu ya kufukizia ubani utaiweka mbele ya sanduku la ushuhuda, kisha utatundika pazia kwenye mlango wa hema takatifu.

6. Ile madhabahu ya kuteketezea sadaka utaiweka mbele ya mlango wa hema takatifu la mkutano.

7. Birika la kutawadhia utaliweka katikati ya hema la mkutano na madhabahu na kulijaza maji.

Kusoma sura kamili Kutoka 40