Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 39:36-42 Biblia Habari Njema (BHN)

36. meza na vyombo vyake vyote, mikate iliyowekwa mbele ya Mungu;

37. kinara cha taa cha dhahabu safi, taa zake, vyombo vyake vyote pamoja na mafuta kwa ajili ya taa hizo;

38. madhabahu ya dhahabu; mafuta ya kupaka, ubani wenye harufu nzuri, na pazia la mlango wa hema;

39. madhabahu ya shaba na wavu wake wa shaba, mipiko yake na vyombo vyake vyote; bakuli, birika na tako lake;

40. vyandarua vya ua, nguzo zake na vikalio vyake; pazia la mlango wa ua, kamba zake na vigingi vyake; vyombo vyote vilivyohitajika katika huduma ya hema takatifu, yaani hema la mkutano;

41. na mavazi yote yaliyofumwa vizuri kabisa kwa ajili ya huduma ya mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu ya kuhani Aroni, na ya wanawe kwa ajili ya huduma ya ukuhani.

42. Waisraeli walifanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Kusoma sura kamili Kutoka 39