Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 38:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Alitengeneza madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa. Madhabahu hiyo ilikuwa ya mraba, mita mbili na robo kwa mita 2.25, na kimo chake mita 1.25.

2. Katika kila pembe ya madhabahu hiyo alitengeneza upembe uliokuwa umeundwa kutokana na madhabahu yenyewe. Madhabahu hiyo yote aliipaka shaba.

3. Alitengeneza pia vyombo vyote kwa ajili ya madhabahu: Vyungu, sepetu, mabirika, nyuma na visahani vya kuchukulia moto. Vyombo vyake vyote alivitengeneza kwa shaba.

4. Alitengeneza wavu wa shaba, akautia chini ya ukingo wa madhabahu hadi katikati ya madhabahu.

5. Katika pembe nne alitengeneza pete nne za kuibebea hiyo madhabahu.

6. Alitengeneza mipiko ya mjohoro na kuipaka shaba.

Kusoma sura kamili Kutoka 38