Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 37:15-29 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Alitengeneza mipiko miwili ya mjohoro ya kulibebea, akaipaka dhahabu.

16. Alitengeneza vyombo vya dhahabu safi vya kuweka juu ya meza: Sahani zake na visahani kwa ajili ya ubani, na bilauri zake na bakuli kwa ajili ya tambiko za kinywaji.

17. Alitengeneza pia kinara cha taa kwa dhahabu safi. Tako lake, na ufito wa hicho kinara ulikuwa kitu kimoja pamoja na vikombe vyake, matumba yake na maua yake.

18. Matawi sita yalitokeza kila upande wa ufito wake, matawi matatu upande mmoja na matawi matatu upande mwingine.

19. Katika kila tawi kulikuwa na vikombe vitatu mfano wa maua ya mlozi, kila kimoja na tumba lake na ua lake.

20. Na katika ufito kulikuwa na vikombe vinne mfano wa maua ya mlozi, pamoja na matumba yake na maua yake.

21. Mahali pale palipotokezea jozi tatu za matawi chini ya kila jozi kulikuwa na tumba moja.

22. Matumba hayo na matawi vilikuwa kitu kimoja na kinara hicho, na chote kilifuliwa kwa dhahabu safi.

23. Alikitengenezea taa saba, koleo na visahani vyake kwa dhahabu safi.

24. Alikitengeneza kinara hicho na vifaa vyake kwa kilo thelathini na tano za dhahabu.

25. Alitengeneza madhabahu ya kufukizia ubani kwa mbao za mjohoro. Madhabahu hiyo ilikuwa ya mraba, sentimita 45 kwa sentimita 45, na kimo chake sentimita 90. Pembe za madhabahu hiyo zilikuwa kitu kimoja na madhabahu yenyewe.

26. Yote aliipaka dhahabu safi: Upande wake wa juu, pande zake za ubavuni na pembe zake; pia aliitengenezea ukingo wa dhahabu.

27. Alitengeneza pete mbili za dhahabu chini ya ukingo kwenye pande mbili zinazokabiliana. Pete hizo zilitumika kushikilia mipiko ya kuibebea.

28. Alifanya mipiko miwili ya mjohoro na kuipaka dhahabu.

29. Alitengeneza mafuta matakatifu ya kupaka, na ubani safi wenye harufu nzuri uliochanganywa vizuri kama manukato.

Kusoma sura kamili Kutoka 37