Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 37:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Bezaleli alitengeneza sanduku kwa mbao za mjohoro; urefu wake ulikuwa sentimita 110, upana sentimita 66, na kimo chake sentimita 66.

2. Alilipaka dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu pande zote.

3. Kisha alitengeneza pete nne za dhahabu za kulibebea, akazitia kwenye pembe zake, kila pembe pete moja.

4. Alitengeneza mipiko ya mjohoro na kuipaka dhahabu.

5. Mipiko hiyo akaipitisha katika zile pete zilizo katika pande mbili za sanduku, kwa ajili ya kulibebea.

Kusoma sura kamili Kutoka 37