Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 36:21-33 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Kila ubao ulikuwa na urefu wa mita 4 na upana wa sentimita 66.

22. Kila ubao ulikuwa na ndimi mbili za kuunganishia. Mbao zote za hema alizifanyia ndimi.

23. Mbao hizo za hema zilitengenezwa hivi: Mbao ishirini upande wa kusini,

24. na vikalio arubaini vya fedha chini ya hizo mbao 20; vikalio viwili chini ya kila ubao ili kushikilia zile ndimi zake mbili.

25. Na upande wa pili, yaani kaskazini mwa hema, alitengeneza pia mbao ishirini,

26. na vikalio vyake arubaini vya fedha; vikalio viwili chini ya kila ubao.

27. Upande wa nyuma, yaani magharibi mwa hema, alitengeneza mbao sita.

28. Alitengeneza pia mbao mbili kwa ajili ya pembe za hema upande wake wa nyuma.

29. Mbao hizo mbili za pembeni ziliachana chini lakini zilishikamanishwa kwenye pete ya kwanza. Mbao mbili kwa ajili ya hizo pembe mbili zilitengenezwa namna hiyo.

30. Hivyo kulikuwa na mbao nane na vikalio vyake vya fedha kumi na sita, vikalio viwili chini ya kila ubao.

31. Alitengeneza pia pau za mjohoro: Pau tano kwa ajili ya mbao za upande mmoja wa hema,

32. pau tano kwa ajili ya upande wa pili wa hema, na pau tano kwa ajili ya mbao za upande wa nyuma wa hema, ulio magharibi.

33. Alitengeneza upau wa katikati uliofika nusu ya jengo la hema ambao ulipenya katikati kutoka mwisho hadi mwisho.

Kusoma sura kamili Kutoka 36