Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 36:13-26 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Kisha alitengeneza vifungo hamsini vya dhahabu ili kuunganishia vile vipande viwili vya mapazia; hivyo, hema likawa kitu kimoja.

14. Kisha alitengeneza pia kifuniko cha hema kwa mapazia kumi na moja ya manyoya ya mbuzi.

15. Kila pazia lilikuwa na urefu wa mita 13, na upana wa mita 2. Mapazia yote 11 yalikuwa ya kipimo kilekile.

16. Basi, akayaunganisha mapazia matano pamoja, na mapazia sita pamoja.

17. Kisha alifanya vitanzi hamsini upindoni mwa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, na vitanzi hamsini upindoni mwa kipande cha pili.

18. Halafu akatengeneza vifungo hamsini vya shaba ili kuunganishia vile vipande viwili vya mapazia, na hivyo kufanya pazia moja la hema.

19. Kisha alitengeneza kifuniko cha ngozi laini ya kondoo dume, na juu yake kifuniko kingine cha ngozi laini ya mbuzi.

20. Halafu akalitengenezea hema mbao za mjohoro za kusimama wima.

21. Kila ubao ulikuwa na urefu wa mita 4 na upana wa sentimita 66.

22. Kila ubao ulikuwa na ndimi mbili za kuunganishia. Mbao zote za hema alizifanyia ndimi.

23. Mbao hizo za hema zilitengenezwa hivi: Mbao ishirini upande wa kusini,

24. na vikalio arubaini vya fedha chini ya hizo mbao 20; vikalio viwili chini ya kila ubao ili kushikilia zile ndimi zake mbili.

25. Na upande wa pili, yaani kaskazini mwa hema, alitengeneza pia mbao ishirini,

26. na vikalio vyake arubaini vya fedha; vikalio viwili chini ya kila ubao.

Kusoma sura kamili Kutoka 36