Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 35:5-20 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Mtatoa katika mali zenu mchango wa kumpa Mwenyezi-Mungu. Kila mtu mwenye moyo mwema atamletea Mwenyezi-Mungu mchango: Dhahabu, fedha, shaba;

6. sufu ya buluu, ya zambarau na nyekundu; kitani safi iliyosokotwa; manyoya ya mbuzi;

7. ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, ngozi za mbuzi; mbao za mjohoro,

8. mafuta kwa ajili ya taa, viungo kwa ajili ya mafuta ya kupaka na kwa ajili ya ubani wenye harufu nzuri;

9. vito vya sardoniki na vito vingine kwa ajili ya mapambo ya kizibao na kifuko cha kifuani.

10. “Kila mtu mwenye ujuzi wa kazi fulani miongoni mwenu atakuja kufanya vitu vyote alivyoamuru Mwenyezi-Mungu:

11. Kutengeneza hema takatifu, kifuniko chake na pazia lake, kulabu zake, pau zake, vikalio vyake;

12. sanduku la agano pamoja na mipiko yake, kiti cha rehema, pazia la mahali patakatifu sana;

13. meza na mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote, mikate iliyowekwa mbele ya Mwenyezi-Mungu;

14. vinara vya taa pamoja na vyombo vyake vyote, taa zake na mafuta yake;

15. madhabahu ya ubani na mipiko yake, mafuta ya kupaka na ubani wenye harufu nzuri, pazia la mlango wa hema takatifu;

16. madhabahu ya sadaka za kuteketezwa pamoja na wavu wa shaba, mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote, birika na tako lake;

17. vyandarua vya ua, nguzo zake na vikalio vyake, pazia la mlango wa ua;

18. vigingi vya hema takatifu na vya ua pamoja na kamba zake;

19. mavazi yaliyofumwa vizuri kabisa kwa ajili ya huduma ya mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu ya kuhani Aroni na ya wanawe, kwa ajili ya huduma yao ya ukuhani.”

20. Basi, jumuiya yote ya Waisraeli ikaondoka mbele ya Mose.

Kusoma sura kamili Kutoka 35