Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 35:12-24 Biblia Habari Njema (BHN)

12. sanduku la agano pamoja na mipiko yake, kiti cha rehema, pazia la mahali patakatifu sana;

13. meza na mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote, mikate iliyowekwa mbele ya Mwenyezi-Mungu;

14. vinara vya taa pamoja na vyombo vyake vyote, taa zake na mafuta yake;

15. madhabahu ya ubani na mipiko yake, mafuta ya kupaka na ubani wenye harufu nzuri, pazia la mlango wa hema takatifu;

16. madhabahu ya sadaka za kuteketezwa pamoja na wavu wa shaba, mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote, birika na tako lake;

17. vyandarua vya ua, nguzo zake na vikalio vyake, pazia la mlango wa ua;

18. vigingi vya hema takatifu na vya ua pamoja na kamba zake;

19. mavazi yaliyofumwa vizuri kabisa kwa ajili ya huduma ya mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu ya kuhani Aroni na ya wanawe, kwa ajili ya huduma yao ya ukuhani.”

20. Basi, jumuiya yote ya Waisraeli ikaondoka mbele ya Mose.

21. Kila mtu aliyevutwa na kusukumwa moyoni mwake alimtolea Mungu mchango wake kwa ajili ya hema la mkutano, huduma zake zote na mavazi yake matakatifu.

22. Hivyo wote wenye moyo mkarimu, wanaume kwa wanawake, wakaleta vipini, pete za mhuri, vikuku na kila aina ya vyombo vya dhahabu; kila mtu akamtolea Mwenyezi-Mungu kitu cha dhahabu.

23. Kila mtu alileta chochote alichokuwa nacho kama vile sufu ya rangi ya buluu zambarau na nyekundu, au kitani safi, au manyoya ya mbuzi au ngozi ya kondoo iliyotiwa rangi nyekundu.

24. Kila mtu aliyeweza kutoa fedha au shaba aliileta kwa Mwenyezi-Mungu kama toleo lake. Tena mtu yeyote aliyekuwa na mbao za mjohoro alileta pia.

Kusoma sura kamili Kutoka 35