Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 31:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,

2. “Mimi nimemteua Bezaleli, mwana wa Uri, mjukuu wa Huri, wa kabila la Yuda

3. na kumjaza roho wangu. Nimempatia uzoefu na akili, maarifa na ufundi,

4. ili abuni kazi za usanii na kufanya kazi za kufua dhahabu, fedha na shaba.

5. Nimempatia ujuzi wa kuchonga mawe ya kupambia, kuchonga mbao, na ujuzi wa kila aina ya ufundi.

6. Vilevile nimemteua Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, afanye kazi pamoja naye. Hali kadhalika nimewapa uwezo mkubwa watu wengine kwa ajili ya kazi mbalimbali, ili watengeneze vifaa vyote nilivyoagiza vifanywe:

7. Hema la mkutano, sanduku la ushuhuda na kiti cha ushuhuda juu yake, pamoja na vifaa vyake vyote;

Kusoma sura kamili Kutoka 31