Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 26:14-27 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Utatengeneza pia kifuniko kingine cha hema kilichofanywa kwa ngozi laini ya kondoo dume na ngozi laini ya mbuzi.

15. “Utatengeneza mbao za mjohoro za kusimama wima kwa ajili ya hema.

16. Kila ubao utakuwa na urefu wa mita 4, na upana wa sentimita 66.

17. Kila ubao utakuwa na ndimi mbili za kuunganishia. Utazifanyia mbao zote ndimi mbili.

18. Basi, utatengeneza hizo mbao za hema hivi: Mbao ishirini kwa ajili ya upande wa kusini,

19. na vikalio arubaini vya fedha chini ya hizo mbao ishirini, vikalio viwili chini kwa kila ubao ili kushikilia zile ndimi zake mbili na vikalio viwili viwe chini ya ubao mwingine ili kushikilia zile ndimi zake mbili.

20. Upande wa kaskazini wa hema, utatengeneza mbao ishirini,

21. na vikalio vyake arubaini vya fedha, vikalio viwili chini ya kila ubao.

22. Kwa upande wa nyuma, ulio magharibi ya hema, utatengeneza mbao sita.

23. Utatengeneza pia mbao mbili kwa ajili ya pembe za hema upande wake wa nyuma.

24. Mbao hizo za pembeni ziachane chini lakini zishikamanishwe kwa juu kwenye pete ya kwanza. Mbao zote za pembeni zifanywe vivyo hivyo ili zifanye pembe mbili.

25. Hivyo kutakuwa na mbao nane pamoja na vikalio vyake kumi na sita vya fedha: Vikalio viwili chini ya kila mbao na vikalio viwili chini ya ubao mwingine.

26. “Utatengeneza pau za mjohoro; pau tano kwa ajili ya mbao za upande mmoja wa hema,

27. na pau tano kwa ajili ya upande wa pili wa hema, na pau tano kwa ajili ya mbao za upande wa nyuma wa hema, ulio magharibi.

Kusoma sura kamili Kutoka 26