Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 26:10-22 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Kisha utafanya vitanzi hamsini upindoni mwa pazia la mwisho la kipande cha kwanza, na vitanzi hamsini upindoni mwa pazia la mwisho la kipande cha pili.

11. Utatengeneza kulabu hamsini za shaba na kuziingiza katika vile vitanzi hamsini ili kuunganishia vile vipande viwili vya mapazia na hivyo kufanya pazia moja la hema.

12. Ile nusu ya pazia iliyobaki utaitundika upande wa nyuma wa hema.

13. Nusu mita ya urefu wa mapazia iliyo ya ziada utaikunja ininginie pande zote mbavuni mwa hema ili kulifunika.

14. Utatengeneza pia kifuniko kingine cha hema kilichofanywa kwa ngozi laini ya kondoo dume na ngozi laini ya mbuzi.

15. “Utatengeneza mbao za mjohoro za kusimama wima kwa ajili ya hema.

16. Kila ubao utakuwa na urefu wa mita 4, na upana wa sentimita 66.

17. Kila ubao utakuwa na ndimi mbili za kuunganishia. Utazifanyia mbao zote ndimi mbili.

18. Basi, utatengeneza hizo mbao za hema hivi: Mbao ishirini kwa ajili ya upande wa kusini,

19. na vikalio arubaini vya fedha chini ya hizo mbao ishirini, vikalio viwili chini kwa kila ubao ili kushikilia zile ndimi zake mbili na vikalio viwili viwe chini ya ubao mwingine ili kushikilia zile ndimi zake mbili.

20. Upande wa kaskazini wa hema, utatengeneza mbao ishirini,

21. na vikalio vyake arubaini vya fedha, vikalio viwili chini ya kila ubao.

22. Kwa upande wa nyuma, ulio magharibi ya hema, utatengeneza mbao sita.

Kusoma sura kamili Kutoka 26