Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 25:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,

2. “Waambie Waisraeli wanipe michango ya matoleo, nawe upokee kwa niaba yangu. Utapokea kutoka kwa mtu yeyote atakayetoa kwa moyo mkunjufu.

3. Utapokea matoleo yafuatayo: Dhahabu, fedha, shaba,

4. sufu ya buluu, ya zambarau na nyekundu, kitani safi iliyosokotwa manyoya ya mbuzi;

5. ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, ngozi za mbuzi, mbao za mjohoro,

6. mafuta kwa ajili ya taa, viungo kwa ajili ya mafuta ya kuweka wakfu na kwa ajili ya ubani wenye harufu nzuri,

7. vito vya sardoniki, na vito vingine kwa ajili ya mapambo ya kizibao cha kuhani na kifuko cha kifuani.

8. Vilevile Waisraeli watanitengenezea hema takatifu, ili niweze kukaa kati yao.

9. Utatengeneza hema hiyo na vifaa vyake kulingana na mfano nitakaokuonesha.

10. “Waisraeli watengeneze sanduku la mbao za mjohoro, lenye urefu wa sentimita 110, upana sentimita 66, na kimo sentimita 66.

11. Utalipaka sanduku hilo dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu pande zote.

Kusoma sura kamili Kutoka 25