Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 19:19-25 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Sauti ya mbiu ilizidi kuongezeka, na Mose akaongea na Mungu. Mungu naye akamjibu katika ngurumo.

20. Mwenyezi-Mungu alishuka juu ya mlima Sinai, akamwita Mose kutoka huko juu, naye Mose akapanda mlimani.

21. Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Shuka chini ukawaonye watu wote wasije kunitazama; la sivyo wengi wao wataangamia.

22. Hata makuhani ambao hunikaribia wanapaswa kujitakasa; la sivyo nitawaadhibu.”

23. Mose akamwambia Mwenyezi-Mungu, “Watu hawa hawawezi kuupanda mlima wa Sinai kwani wewe mwenyewe ulituamuru tuweke mpaka kuuzunguka mlima.”

24. Mwenyezi-Mungu akasema, “Teremka chini kisha urudi pamoja na Aroni. Lakini usiwaruhusu makuhani na watu wengine wapite mpaka na kuja kwangu, la sivyo nitawaadhibu.”

25. Basi, Mose akashuka na kuwaambia Waisraeli mambo yote aliyoagizwa.

Kusoma sura kamili Kutoka 19