Agano la Kale

Agano Jipya

Kutoka 1:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Haya ndiyo majina ya watoto wa kiume wa Israeli, ambao walikwenda Misri, kila mmoja na jamaa yake:

2. Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda,

3. Isakari, Zebuluni, Benyamini,

4. Dani, Naftali, Gadi na Asheri.

5. Wazawa wote wa Yakobo walikuwa watu 70. Wakati huo Yosefu alikuwa amekwisha tangulia kukaa huko Misri.

6. Baadaye, Yosefu alifariki, hali kadhalika ndugu zake na kizazi kile chote.

7. Lakini wazawa wa Israeli waliongezeka sana, wakawa wengi na wenye nguvu mno, wakaenea kila mahali nchini Misri.

8. Basi, akatokea mfalme mwingine huko Misri ambaye hakumjua Yosefu.

9. Naye akawaambia watu wake, “Tazameni jinsi Waisraeli walivyo wengi na wenye nguvu kuliko sisi.

10. Ni lazima tutafute hila ya kuwapunguza na kuzuia wasiongezeke; la sivyo, kama vita vikitokea watajiunga na adui zetu na kuitoroka nchi.”

11. Basi, Wamisri wakawateua wanyapara wawasimamie Waisraeli na kuwatesa kwa kazi ngumu. Waisraeli wakafanya kazi ya kumjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.

12. Lakini kadiri walivyoteswa ndivyo Waisraeli walivyozidi kuongezeka na kuenea nchini. Hivyo Wamisri wakawaogopa sana watu wa Israeli.

13. Basi, Wamisri wakawatumikisha Waisraeli kikatili,

Kusoma sura kamili Kutoka 1