Agano la Kale

Agano Jipya

Kumbukumbu La Sheria 7:18-26 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Msiwaogope, kumbukeni vile Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alivyomtendea Farao na nchi nzima ya Misri.

19. Kumbukeni maradhi mabaya mliyoyaona kwa macho yenu, miujiza na maajabu na nguvu kubwa na uwezo mkuu, ambavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; alitumia kuwakomboa; hivyo ndivyo atakavyowatenda watu mnaowaogopa.

20. Zaidi ya hayo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atapeleka mavu kati yao na kuwaangamiza wale ambao watawatoroka ili kujificha.

21. Basi, msiwaogope, kwa sababu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, yuko kati yenu. Yeye ni Mungu mkuu na wa kutisha.

22. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atayafukuza mataifa haya kadiri mnavyosonga mbele kidogokidogo. Hamtaweza kuyaangamiza yote kwa mara moja, kwa sababu mkifanya hivyo idadi ya wanyama wa porini itazidi na kuwa tisho kwenu.

23. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawatia adui zenu mikononi mwenu na atawafanya wahangaike mpaka waangamie.

24. Atawatia wafalme wao mikononi mwenu. Mtawaua, nao watasahaulika. Hakuna mtu yeyote atakayeweza kuwazuia, mpaka mtakapowaangamiza.

25. Teketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga za miungu yao. Msitamani fedha wala dhahabu yao, wala msiichukue na kuifanya mali yenu. Kufanya hivyo ni mtego kwenu na ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.

26. Msipeleke nyumbani kwenu kitu chochote cha kuchukiza, la sivyo mtalaaniwa kama hicho kitu. Ni lazima mkichukie na kukidharau kabisa kwa kuwa ni kitu kilicholaaniwa.

Kusoma sura kamili Kumbukumbu La Sheria 7