Agano la Kale

Agano Jipya

Kumbukumbu La Sheria 5:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)

6. “ ‘Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya Misri, ambako ulikuwa mtumwa.

7. “ ‘Usiwe na miungu mingine ila mimi.

8. “ ‘Usijifanyie sanamu za miungu za kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

9. “ ‘Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wale wanichukiao.

10. Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.

11. “ ‘Usilitaje bure jina langu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; maana mimi ni Mwenyezi-Mungu sitaacha kumwadhibu yeyote afanyaye hivyo.

Kusoma sura kamili Kumbukumbu La Sheria 5