Agano la Kale

Agano Jipya

Kumbukumbu La Sheria 33:18-28 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Juu ya kabila la Zebuluni na kabila la Isakari, alisema,“Zebuluni, furahi katika safari zako;nawe Isakari, furahi katika mahema yako.

19. Watawaalika wageni kwenye milima yao,na huko watu watatoa sadaka zinazotakiwa.Maana wao watapata utajiri wao kutoka baharinina hazina zao katika mchanga wa pwani.”

20. Juu ya kabila la Gadi, alisema:“Atukuzwe Mungu ampatiaye Gadi sehemu kubwa.Gadi hunyemelea kama simbaakwanyue mkono na utosi wa kichwa.

21. Alijichagulia eneo zuri kuliko yote,mahali ilipotengwa sehemu ya kiongozi.Aliwaongoza watu na kumtii Mwenyezi-Mungu,alitekeleza mpango wa Mungu kwa Israeli.”

22. Juu ya kabila la Dani alisema hivi:“Dani ni mwanasimbaarukaye kutoka Bashani.”

23. Juu ya kabila la Naftali alisema:“Ee Naftali fadhili,uliyejaa baraka za Mwenyezi-Mungu,nchi yako ni kusini kwenye ziwa Kinerethi.”

24. Juu ya kabila la Asheri alisema:“Asheri abarikiwe kuliko watoto wote wa Yakobo,na upendelewe na ndugu zako wote;na achovye mguu wake katika mafuta.

25. Miji yako ni ngome za chuma na shaba.Usalama wako utadumu maisha yako yote!”

26. Mose akamalizia kwa kusema,“Ee Israeli, hakuna aliye kama Mungu wako,yeye hupita mbinguni kuja kukusaidia,hupita juu angani katika utukufu wake.

27. Mungu wa milele ndiye kimbilio lenu;nguvu yake yaonekana duniani.Aliwafukuza maadui mbele yenu;aliwaamuru: ‘Waangamizeni.’

28. Kwa hiyo, watu wa Israeli wakakaa salama,wazawa wa Yakobo peke yao,katika nchi iliyojaa nafaka na divai,nchi ambayo anga lake hudondosha umande.

Kusoma sura kamili Kumbukumbu La Sheria 33