Agano la Kale

Agano Jipya

Kumbukumbu La Sheria 33:11-17 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Ee Mwenyezi-Mungu, uzibariki nguvu zao,uzikubali kazi za mikono yao;uzivunjilie mbali nguvu za maadui zao,nguvu za wanaowachukia hata wasiinuke tena.”

12. Juu ya kabila la Benyamini alisema:“Hili ni kabila alipendalo Mwenyezi-Mungu,nalo hukaa salama karibu naye.Yeye hulilinda mchana kutwa,na kukaa kati ya milima yake.”

13. Juu ya kabila la Yosefu alisema:“Mwenyezi-Mungu na aibariki nchi yake,kwa baraka nzuri kabisa kutoka juu,

14. ibarikiwe kwa matunda bora yalioiva kwa jua,kwa matunda ya kila mwezi;

15. kwa mazao bora ya milima ya kale,na mazao tele ya milima ya kale,

16. Nchi yake ijae yote yaliyo mema,ibarikiwe kwa wema wa Mwenyezi-Mungu,ambaye alitokea katika kichaka.Baraka hizi ziwashukie watu wa kabila la Yosefu,aliyekuwa mkuu miongoni mwa ndugu zake.

17. Fahari yake ni fahari ya fahali wa kwanza,pembe zake ni za nyati dume.Atazitumia kuyasukuma mataifa;yote atayasukuma mpaka miisho ya dunia.Efraimu atakuwa na pembe hizo 10,000na Manase kwa maelfu.”

Kusoma sura kamili Kumbukumbu La Sheria 33