Agano la Kale

Agano Jipya

Kumbukumbu La Sheria 29:9-18 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Kwa hiyo muwe waangalifu kushika maneno yote ya agano hili ili mpate kufanikiwa katika kazi zenu zote.

10. “Leo, mmesimama mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nyinyi nyote viongozi wa makabila, wazee wenu, maofisa wenu,

11. watoto wenu na wake zenu, wageni wanaoishi miongoni mwenu ambao hukata kuni na kuwatekea maji.

12. Mko hapa leo ili kufanya agano hili ambalo Bwana Mungu wenu anafanya leo,

13. kwamba atawathibitisha leo kuwa watu wake naye atakuwa Mungu wenu, kama alivyowaapia nyinyi na babu zenu: Abrahamu, Isaka na Yakobo.

14. Wala sifanyi agano hili leo kwa niaba yenu tu na kutamka laana zake; sifanyi kwa niaba ya wale tu walio pamoja nasi leo mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,

15. bali pia kwa niaba ya wale ambao hawapo pamoja nasi leo.

16. “Mnajua jinsi tulivyoishi nchini Misri na jinsi tulivyosafiri katika nchi za mataifa mengine.

17. Mliona sanamu zao za kuchukiza, miungu ya miti na mawe, ya fedha na dhahabu.

18. Chukueni hadhari kwamba hakuna mwanamume, mwanamke, jamaa au kabila lolote linalosimama hapa leo litakalomwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kwenda kutumikia miungu ya mataifa mengine. Jambo hili litakuwa kama mzizi utakaomea na kuzaa matunda machungu yenye sumu.

Kusoma sura kamili Kumbukumbu La Sheria 29