Agano la Kale

Agano Jipya

Kumbukumbu La Sheria 20:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Mkienda vitani kupigana na adui zenu, mkaona farasi, magari na jeshi kubwa zaidi kuliko lenu msiwaogope. Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliyewatoa Misri, atakuwa nanyi.

2. Kabla ya kuanza mapigano, kuhani atajitokeza mbele na kuwaambia watu,

3. ‘Watu wa Israeli sikilizeni! Leo mnakaribia kupigana dhidi ya adui zenu. Msife moyo, au kuogopa, au kutishika, au kuwaogopa adui;

4. maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ndiye atakayekwenda pamoja nanyi kupigana kwa niaba yenu dhidi ya adui zenu na kuwapa ushindi.’

Kusoma sura kamili Kumbukumbu La Sheria 20