1. “Nyinyi ni watoto wa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; msijichanje wala kunyoa upara kwa ajili ya mtu aliyefariki.
2. Nyinyi ni watu watakatifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; Mwenyezi-Mungu amewachagua muwe watu wake hasa, kati ya watu wote waishio duniani.
3. “Msile kitu kilicho chukizo kwa Mungu.
4. Mnaweza kula wanyama wafuatao: Ng'ombe, kondoo, mbuzi,
5. kulungu, paa, kongoni, mbuzimwitu, paa mweupe, pofu na mbuzi wa mlimani;
6. na kila mnyama mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na mwenye kucheua, huyo mnaweza kula.