Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 8:11-19 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Mwenyezi-Mungu alinionya kwa nguvu nisifuate njia za watu hawa, akaniambia,

12. “Usijumuike nao katika njama zao, wala usiogope yale wanayoyaogopa wala kuwa na hofu.

13. Nitambue mimi peke yangu, Mwenyezi-Mungu wa majeshi, kuwa mtakatifu; utaniogopa na kunicha mimi peke yangu.

14. Mimi nitakuwa kimbilio, nitakuwa pia kama jiwe la kujikwaa, mwamba wa kuziangusha falme za Israeli na Yuda; nitakuwa mtego wa kuwatega na kuwanasa wakazi wa Yerusalemu.

15. Watu wengi watajikwaa, wataanguka na kupondeka; watanaswa katika mtego huo na kuchukuliwa mateka.”

16. Nitalihifadhi agizo hilo na kulifunga fundisho hilo miongoni mwa wafuasi wangu.

17. Nitamngojea Mwenyezi-Mungu ambaye amejificha mbali na wazawa wa Yakobo; nitamtumainia.

18. Mimi pamoja na watoto alionipa Mwenyezi-Mungu ni ishara na alama katika Israeli kwa jina la Mwenyezi-Mungu wa majeshi akaaye mlimani Siyoni.

19. Baadhi watawaambieni: “Nendeni mkatake shauri kwa mizimu na mizuka iliayo kama ndege; kwani ni kawaida watu kutaka shauri kwa miungu yao, na kutaka shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai.”

Kusoma sura kamili Isaya 8