Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 64:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Wakati ulipotenda maajabu ambayo hatukutazamia,ulishuka chini nayo milima ikatetemeka ilipokuona.

4. Tangu kale hakuna aliyepata kuonawala kusikia kwa masikio yake;hakuna aliyepata kumwona Mungu aliye kama weweatendaye mambo kwa ajili ya wale wanaomtegemea!

5. Wewe waja kuwasaidia watendao haki kwa furaha,wanaokukumbuka na kuzingatia njia zako.Ulitukasirikia tulipokuwa wenye dhambi;sisi tumeasi kwa muda mrefu.

6. Sote tumekuwa kama watu walio najisi;matendo yetu yote mema ni kama nguo chafu.Sote tunanyauka kama majani,uovu wetu watupeperusha kama upepo.

Kusoma sura kamili Isaya 64