Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 63:7-12 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Nitasimulia fadhili za Mwenyezi-Mungu;nitataja matendo yake yote yastahiliyo sifa,kwa sababu ya yote aliyotutendea,wema wake mkuu aliowapa Waisraeli kwa huruma yake,kadiri ya wingi wa fadhili zake.

8. Maana alisema juu yao:“Hakika, hawa ni watu wangu;watoto wangu ambao hawatanidanganya.”Basi yeye akawa Mwokozi wao.

9. Katika taabu zao zote,hakumtuma mjumbe mwingine kuwasaidia,ila yeye mwenyewe alikuja kuwaokoa.kwa upendo na huruma yake aliwakomboa.Aliwabeba na kuwachukua tangu zamani.

10. Lakini wao walikuwa wakaidi,wakaihuzunisha roho yake takatifu.Basi, Mungu akageuka, akawa adui yao;yeye mwenyewe akapigana nao.

11. Ndipo walipokumbuka siku za zamani,wakati wa Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu.Wakauliza, “Yuko wapi sasa Mwenyezi-Mungu,aliyewaokoa wachungaji wa kundi lake baharini?Yuko wapi yule aliyeiweka roho yake takatifu kati yao,

12. ambaye kwa mkono wake wenye nguvualifanya maajabu kwa njia ya Mose,akapasua bahari na kuwaongoza watu wake,na kujipatia jina la milele?

Kusoma sura kamili Isaya 63