Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 63:11-19 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Ndipo walipokumbuka siku za zamani,wakati wa Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu.Wakauliza, “Yuko wapi sasa Mwenyezi-Mungu,aliyewaokoa wachungaji wa kundi lake baharini?Yuko wapi yule aliyeiweka roho yake takatifu kati yao,

12. ambaye kwa mkono wake wenye nguvualifanya maajabu kwa njia ya Mose,akapasua bahari na kuwaongoza watu wake,na kujipatia jina la milele?

13. Aliwaongoza katikati ya vilindi vya bahari,wakapita humo kama farasi bila kujikwaa.

14. Kama ng'ombe wapelekwavyo malishoni bondeni,ndivyo roho ya Mungu ilivyowapumzisha watu wake.Ndivyo ee Mungu ulivyowaongoza watu wako,nawe ukajipatia jina tukufu.”

15. Ututazame kutoka mbinguni ee Mungu, uone,utuangalie kutoka makao yako matakatifu na matukufu.Iko wapi bidii yako kwa ajili yetu na nguvu yako?Usiache kutuonesha upendo wako.

16. Maana wewe ndiwe Baba yetu;Abrahamu, mzee wetu, hatujali,naye Israeli hatutambui;lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ni Baba yetu.Wewe umeitwa tangu kale: “Mkombozi wetu.”

17. Ee Mwenyezi-Mungu, mbona unatukosesha njia zako?Mbona unatufanya kuwa wakaidi hata tusikuogope?Rudi ee Mungu kwa ajili ya watumishi wako,makabila ambayo daima yalikuwa mali yako.

18. Kwa kitambo tu sisi watakatifu wako tulimiliki nchi,lakini maadui zetu wakaja wakaharibu maskani yako.

19. Tumekuwa kama watu ambao hujawatawala kamwe,kama watu ambao hawakujulikana kwa jina lako.

Kusoma sura kamili Isaya 63