Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 62:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Maana kama kijana mwanamume amwoavyo msichana,ndivyo aliyekujenga atakavyokuwa mume wako.Kama bwana arusi afurahivyo juu ya bibi arusi,ndivyo Mungu atakavyofurahi juu yako.

6. “Juu ya kuta zako ee Yerusalemu nimeweka walinzi,usiku na mchana kamwe hawatakaa kimya.”Enyi mnaomkumbusha Mwenyezi-Mungu ahadi yake,msikae kimya;

7. msimpe hata nafasi ya kupumzika,mpaka atakapousimika mji wa Yerusalemu,na kuufanya uwe fahari ulimwenguni kote.

8. Mwenyezi-Mungu ameapa kwa mkono wake wa kulia,naam, ameapa kwa mkono wake wenye nguvu akisema:“Sitawapa tena maadui zako nafaka yako;wala wageni hawatakunywa tena divai yakoambayo umeitolea jasho.

9. Bali nyinyi mliyoivuna nafaka hiyo,mtaila na kunitukuza mimi Mwenyezi-Mungu.Nyinyi mliochuma zabibu hizo,mtakunywa divai yake katika nyua zangu takatifu.”

10. Wakazi wa Yerusalemu, tokeni, tokeni nje ya mji,watayarishieni njia watu wenu wanaorejea!Jengeni! Jengeni barabara na kuondoa mawe yote!Wekeni alama kwa ajili ya watu.

11. Mwenyezi-Mungu ametangaza duniani kote,waambie watu wa Siyoni:“Mkombozi wenu anakuja,zawadi yake iko pamoja nayena tuzo lake liko mbele yake.”

12. Nyinyi mtaitwa: “Watu Watakatifu”,“Watu waliokombolewa na Mwenyezi-Mungu.”Na Yerusalemu utaitwa: “Mji aupendao Mungu”,“Mji ambao Mungu hakuuacha.”

Kusoma sura kamili Isaya 62