Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 61:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Bwana Mwenyezi-Mungu amenijaza roho yake,maana Mwenyezi-Mungu ameniweka wakfu,akanituma niwaletee wanaokandamizwa habari njema,niwatibu waliovunjika moyo,niwatangazie mateka kwamba watapata uhuru,na wafungwa kwamba watafunguliwa.

2. Amenituma niutangaze mwaka wake wa neema,na siku ya Mungu wetu ya kulipiza kisasi;niwafariji wote wanaoomboleza;

3. niwape wale wanaoomboleza katika Siyonitaji la maua badala ya majivu,mafuta ya furaha badala ya maombolezo,vazi la sifa badala ya moyo mzito.Nao wataitwa mialoni madhubuti,aliyopanda Mwenyezi-Mungu kuonesha utukufu wake.

4. Watayajenga upya magofu ya zamani,wataisimika miji iliyoharibiwa hapo kwanza;wataitengeneza miji iliyobomolewa,uharibifu wa vizazi vingi vilivyopita.

5. Wageni watakuwa hapo kuwachungia mifugo yenu;watawalimia na kuwatunzia mizabibu yenu.

Kusoma sura kamili Isaya 61