Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 60:8-11 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Nani hao wanaopepea kama mawingu,kama njiwa wanaoruka kwenda viotani mwao?

9. Ni meli zitokazo nchi za mbali,zikitanguliwa na meli za Tarshishi.Zinawaleta watoto wako,pamoja na fedha na dhahabu yao,kwa sifa ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako,kwa sifa ya Mungu, Mtukufu wa Israeli,maana amewafanya mtukuke.

10. Mwenyezi-Mungu asema:“Wageni watazijenga upya kuta zako,wafalme wao watakutumikia.Maana kwa hasira yangu nilikupiga,lakini kwa fadhili yangu nimekuhurumia.

11. Malango yako yatakuwa wazi daima;usiku na mchana hayatafungwa,ili watu wakuletee utajiri wa mataifa,pamoja na wafalme wao katika maandamano.

Kusoma sura kamili Isaya 60