Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 60:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Inuka ee Siyoni uangaze;maana mwanga unachomoza kwa ajili yako,utukufu wa Mwenyezi-Mungu unakuangaza.

2. Tazama, giza litaifunika dunia,giza nene litayafunika mataifa;lakini wewe, Mwenyezi-Mungu atakuangazia,utukufu wake utaonekana kwako.

3. Mataifa yataujia mwanga wako,wafalme waujia mwanga wa pambazuko lako.

4. Inua macho utazame pande zote;wote wanakusanyika waje kwako.Wanao wa kiume watafika toka mbali,wanao wa kike watabebwa mikononi.

5. Utaona na uso wako utangara,moyo wako utasisimka na kushangilia.Maana utajiri wa bahari utakutiririkia,mali za mataifa zitaletwa kwako.

6. Makundi ya ngamia yataifunika nchi yako,naam, ndama wa ngamia kutoka Midiani na Efa;wote kutoka Sheba watakuja.Watakuletea dhahabu na ubani,wakitangaza sifa za Mwenyezi-Mungu.

7. Makundi ya kondoo wa Kedari yatakusanywa kwako,utaweza kuwatumia kondoo madume wa Nebayothi kuwa kafara;utawatoa kuwa tambiko inayokubalika madhabahuni pa Mungu,naye ataitukuza nyumba yake tukufu.

8. Nani hao wanaopepea kama mawingu,kama njiwa wanaoruka kwenda viotani mwao?

Kusoma sura kamili Isaya 60