Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 59:18-21 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Atawaadhibu maadui kadiri ya matendo yao,naam, ghadhabu yake na kisasi vitawapata maadui zake;atawaadhibu hata wakazi wa nchi za mbali.

19. Toka magharibi hadi mashariki,kila mtu atamcha Mwenyezi-Munguna kutambua utukufu wake.Maana atakuja kama mto uendao kasi,mto unaosukumwa kwa upepo wa Mwenyezi-Mungu.

20. Naye atakuja Siyoni kama Mkombozi,Mkombozi wa wazawa wa Yakoboambao wataachana na makosa yao.Asema Mwenyezi-Mungu.

21. Mwenyezi-Mungu asema:“Mimi nafanya nanyi agano hili:Roho yangu niliyowajazeni,maneno niliyoyaweka mdomoni mwenu,hayataondoka kwenu kamwe,wala kwa watoto na wajukuu zenu,tangu sasa na hata milele.”

Kusoma sura kamili Isaya 59