Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 58:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)

6. “La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu:Kuwafungulia waliofungwa bila haki,kuziondoa kamba za utumwa,kuwaachia huru wanaokandamizwa,na kuvunjilia mbali udhalimu wote!

7. Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako,kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao,kuwavalisha wasio na nguo,bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu.

8. “Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko,mkiwa wagonjwa mtapona haraka.Matendo yenu mema yatawatangulia,nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu.

Kusoma sura kamili Isaya 58