Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 58:10-14 Biblia Habari Njema (BHN)

10. mkiwapa chakula kwa ukarimu wenye njaa,mkitosheleza mahitaji ya wenye dhiki,mwanga utawaangazia nyakati za giza,giza lenu litakuwa kama mchana.

11. Mimi Mwenyezi-Mungu nitawaongozeni daima,nitatosheleza mahitaji yenu wakati wa shida.Nitawaimarisha mwilini,nanyi mtakuwa kama bustani iliyomwagiliwa maji,kama chemchemi ya majiambayo maji yake hayakauki kamwe.

12. Magofu yenu ya kale yatajengwa;mtajenga upya juu ya misingi iliyoachwa zamani.Nanyi mtaitwa watu waliotengeneza upya kuta,watu waliozifanya barabara za mji zipitike tena.

13. “Kama ukiacha kufanya kazi siku ya Sabato,ukaacha shughuli zako siku yangu hiyo takatifu;kama ukiifanya siku yangu kuwa ya furaha,ukaiheshimu siku hiyo takatifu ya Mwenyezi-Mungu,ukaacha na shughuli zako na kupiga domo,

14. utapata furaha yako kwangu mimi Mwenyezi-Mungu,nitakupatia ushindi katika kila pingamizi nchini,nitakulisha mali ya Yakobo, babu yako.Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”

Kusoma sura kamili Isaya 58