Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 58:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu asema:“Piga kelele, wala usijizuie;paza sauti yako kama tarumbeta.Watangazie watu wangu makosa yao,waambie wazawa wa Yakobo dhambi zao.

2. Siku hata siku wananijia kuniabudu,wanatamani kujua mwongozo wangu,kana kwamba wao ni taifa litendalo haki,taifa lisilosahau sheria za Mungu wao.Wananitaka niamue kwa haki,na kutamani kukaa karibu na Mungu.

3. “Nyinyi mnaniuliza:‘Mbona tunafunga lakini wewe huoni?Mbona tunajinyenyekesha, lakini wewe hujali?’“Ukweli ni kwamba wakati mnapofunga,mnatafuta tu furaha yenu wenyewe,na kuwakandamiza wafanyakazi wenu!

Kusoma sura kamili Isaya 58