Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 56:6-12 Biblia Habari Njema (BHN)

6. “Watu wageni watakaonikiri mimi Mwenyezi-Mungu,watakaoniheshimu, wakapenda jina langu na kuwa watumishi wangu,wote watakaoshika Sabato bila kuikufuru,watu watakaozingatia agano langu,

7. hao nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu,na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala;tambiko na sadaka zao zitakubaliwa madhabahuni pangu.Maana nyumba yangu itaitwa:‘Nyumba ya sala kwa ajili ya watu wote’.

8. “Hii ni kauli yangu mimi Bwana Mwenyezi-Munguninayewakusanya Waisraeli waliotawanyika.Licha ya hao niliokwisha kukusanya,nitawakusanya watu wengine wajumuike nao.”

9. Enyi wanyama wote wakali,nanyi wanyama wote wa mwituni,njoni muwatafune watu wangu.

10. Maana viongozi wao wote ni vipofu;wote hawana akili yoyote.Wote ni kama mbwa bubu wasiobweka,hulala tu na kuota ndoto,hupenda sana kusinzia!

11. Hao ni kama mbwa wenye uchu sana,wala hawawezi kamwe kutoshelezwa.Wachungaji hao hawana akili yoyote;kila mmoja hutafuta faida yake mwenyewe.

12. Huambiana, “Njoni, twende kutafuta divai;njoni tunywe tushibe pombe!Kesho itakuwa kama leo,tena itakuwa sikukuu kubwa zaidi.”

Kusoma sura kamili Isaya 56