Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 56:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu asema:“Zingatieni haki na kutenda mema,maana nitawaokoeni hivi karibuni,watu wataona wazi kwamba ninawakomboeni.

2. Heri mtu anayezingatia kikamilifu ninayosema,anayeshika sheria ya Sabato kwa heshimana kuepa kutenda uovu wowote.

3. “Mgeni anayenitambua mimi Mwenyezi-Mungu asifikiri:‘Hakika Mwenyezi-Mungu atanitenga na watu wake.’Naye towashi asiseme:‘Mimi ni mti mkavu tu!’

4. Maana mimi Mwenyezi-Mungu nasema:Towashi ashikaye sheria zangu za Sabato,anayefanya mambo yanayonipendeza,na kulizingatia agano langu,

5. nitampa nafasi maalumu na ya sifakatika nyumba yangu na kuta zake;nafasi bora kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike:Nitampa jina la kukumbukwa daima,na ambalo halitafutwa kamwe.

6. “Watu wageni watakaonikiri mimi Mwenyezi-Mungu,watakaoniheshimu, wakapenda jina langu na kuwa watumishi wangu,wote watakaoshika Sabato bila kuikufuru,watu watakaozingatia agano langu,

7. hao nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu,na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala;tambiko na sadaka zao zitakubaliwa madhabahuni pangu.Maana nyumba yangu itaitwa:‘Nyumba ya sala kwa ajili ya watu wote’.

8. “Hii ni kauli yangu mimi Bwana Mwenyezi-Munguninayewakusanya Waisraeli waliotawanyika.Licha ya hao niliokwisha kukusanya,nitawakusanya watu wengine wajumuike nao.”

Kusoma sura kamili Isaya 56