Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 54:2-12 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Panua nafasi hemani mwako,tandaza mapazia hapo unapoishi,usijali gharama zake.Zirefushe kamba zake,na kuimarisha vigingi vyake;

3. maana utapanuka kila upande;wazawa wako watamiliki mataifa,miji iliyokuwa mahame itajaa watu.

4. Usiogope maana hutaaibishwa tena;usifadhaike maana hutadharauliwa tena.Utaisahau aibu ya ujana wako,wala hutaikumbuka tena fedheha ya ujane wako.

5. Muumba wako atakuwa mume wako;Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndilo jina lake,Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako;yeye aitwa ‘Mungu wa ulimwengu wote’.

6. “Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewekama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika,mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa.Mungu wako anasema:

7. Nilikuacha kwa muda mfupi tu;kwa huruma nyingi, nitakurudisha.

8. Kwa hasira nyingi nilikuficha uso wangu kwa kitambo,lakini kwa fadhili za milele nitakuonea huruma.Mimi Mwenyezi-Mungu Mkombozi wako, nimesema.

9. “Nitafanya kama nilivyofanya wakati wa Noa:Wakati ule niliapa kwambasitaifunika tena ardhi kwa gharika.Basi sasa naapa kwamba sitakukasirikia tenawala sitakukemea tena.

10. Milima yaweza kutoweka,vilima vyaweza kuondolewa,lakini fadhili zangu hazitakuondoka,agano langu la amani halitaondolewa.Mimi Mwenyezi-Mungu nikuhurumiaye nimesema.

11. “Ewe Yerusalemu uliyeteseka,uliyetaabishwa na kukosa wa kukufariji!Nitakujenga upya kwa mawe ya thamani,misingi yako itakuwa ya johari ya rangi ya samawati.

12. Minara yako nitaijenga kwa mawe ya akiki,malango yako kwa almasi,na ukuta wako kwa mawe ya thamani.

Kusoma sura kamili Isaya 54