Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 54:11-17 Biblia Habari Njema (BHN)

11. “Ewe Yerusalemu uliyeteseka,uliyetaabishwa na kukosa wa kukufariji!Nitakujenga upya kwa mawe ya thamani,misingi yako itakuwa ya johari ya rangi ya samawati.

12. Minara yako nitaijenga kwa mawe ya akiki,malango yako kwa almasi,na ukuta wako kwa mawe ya thamani.

13. “Watu wako watafunzwa nami Mwenyezi-Mungu,wanao watapata ustawi mwingi.

14. Utaimarika katika uadilifu,utakuwa mbali na dhuluma,nawe hutaogopa kitu;utakuwa mbali na hofu,maana haitakukaribia.

15. Mtu yeyote akija kukushambulia,hatakuwa ametumwa nami.Yeyote atakayekushambulia,ataangamia mbele yako.

16. “Tazama, mimi ndiye niliyemuumba mhunzi,afukutaye moto wa makaa na kufua silaha.Ni mimi pia niliyemuumba mwangamizi anayeangamiza.

17. Silaha zote zilizoundwa kukudhuru wewehazitafaa chochote kile.Mtu akikushtaki mahakamani, utamshinda.Hilo ndilo fungu nililowapangia watumishi wangu.Hizo ndizo haki nilizowathibitishia.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Kusoma sura kamili Isaya 54