Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 52:6-15 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Kwa hiyo watu wangu watajua mimi ni nani; siku hiyo watajua kwamba ni mimi ninayesema: Niko!”

7. Tazama inavyopendezakumwona mjumbe akitokea mlimani,ambaye anatangaza amani,ambaye analeta habari njema,na kutangaza ukombozi!Anauambia mji wa Siyoni:“Mungu wako anatawala!”

8. Sikiliza sauti ya walinzi wako;wanaimba pamoja kwa furaha,maana wanaona kwa macho yao wenyewe,kurudi kwa Mwenyezi-Mungu mjini Siyoni.

9. Pazeni sauti za shangwe, enyi magofu ya Yerusalemu!Mwenyezi-Mungu amewafariji watu wake,ameukomboa mji wa Yerusalemu.

10. Mwenyezi-Mungu ameonesha nguvu yake tukufu,mbele ya mataifa yote.Atawaokoa watu wake,na ulimwengu wote utashuhudia.

11. Ondokeni! Ondokeni! Tokeni hapa;msiguse kitu chochote najisi!Ondokeni huku Babuloni!Jitakaseni enyi mbebao vyombo vya Mwenyezi-Mungu.

12. Safari hii hamtatoka kwa haraka,wala hamtaondoka mbiombio!Maana Mwenyezi-Mungu atawatangulieni,Mungu wa Israeli atawalinda kutoka nyuma.

13. Mungu asema hivi:“Mtumishi wangu atafanikiwa;atatukuzwa na kupewa cheo,atapata heshima kuu.

14. Wengi waliomwona walishtuka,kwa vile sura yake ilikuwa imeharibiwa;hakuwa tena na umbo la kibinadamu!

15. Lakini sasa ameyashangaza mataifa mengi.Wafalme wanaduwaa kwa sababu yake,maana wataona mambo ambayo hawajapata kuambiwa,na kufahamu mambo ambayo hawajapata kusikia.”

Kusoma sura kamili Isaya 52