Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 52:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Amka! Amka!Jipe nguvu zako ewe mji wa Siyoni!Jivike mavazi yako mazuri,ewe Yerusalemu, mji mtakatifu.Maana hawataingia tena kwakowatu wasiotahiriwa na walio najisi.

2. Jikungute mavumbi, uinukeewe Yerusalemu uliyetekwa nyara!Jifungue minyororo yako shingoni,ewe binti Siyoni uliyechukuliwa mateka.

3. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nyinyi mliuzwa utumwani bila malipo yoyote, na mtakombolewa bila kulipa hata senti moja.

4. Tena mwanzoni nyinyi watu wangu mlikimbilia Misri mkakaa huko. Halafu baadaye Waashuru waliwakandamiza bila sababu yoyote.

5. Katika hali ya sasa napata faida gani kuwaona watu wangu wamepelekwa utumwani? Hao wanaowatawala wanajitapa. Nalo jina langu laendelea kudharauliwa kila siku.

6. Kwa hiyo watu wangu watajua mimi ni nani; siku hiyo watajua kwamba ni mimi ninayesema: Niko!”

7. Tazama inavyopendezakumwona mjumbe akitokea mlimani,ambaye anatangaza amani,ambaye analeta habari njema,na kutangaza ukombozi!Anauambia mji wa Siyoni:“Mungu wako anatawala!”

Kusoma sura kamili Isaya 52