Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 51:9-17 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Amka! Amka ee Mwenyezi-Mungu!Jivike nguvu zako utuokoe.Amka kama ulivyofanya hapo zamani,nyakati za vizazi vya hapo kale.Je, si wewe uliyemkatakata Rahabu,ukalitumbua dude hilo la kutisha?

10. Wewe ndiwe uliyeikausha bahari,ndiwe uliyevikausha vilindi vya maji,ukafanya njia katika vilindi vya bahari,ili wale uliowakomboa wavuke humo.

11. Watu wako uliowakomboa, ee Mwenyezi-Mungu, watarudi,watakuja Siyoni wakiimba;watajaa furaha ya milele,watapata furaha na shangwe.Huzuni na maombolezo vitatoweka kabisa.

12. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mimi, naam mimi, ndimi ninayekufariji.Kwa nini wewe unamwogopa mtu ambaye hufa,binadamu ambaye hutoweka kama nyasi?

13. Wewe umenisahau mimi Mwenyezi-Mungu Muumba wako,niliyezitandaza mbingu,na kuiweka misingi ya dunia!Wewe waendelea kuogopa siku zote,kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu wako,kwamba yuko tayari kukuangamiza!Lakini hasira yake itafika wapi?

14. Wanaodhulumiwa watafunguliwa hima,hawatakufa na kushuka shimoni,wala hawatatindikiwa chakula.

15. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wako;nivurugaye bahari, mawimbi yake yakanguruma;Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndilo jina langu!

16. Nimeyaweka maneno yangu mdomoni mwako;nimekuficha katika kivuli cha mkono wangu.Mimi nilizitandaza mbingu,nikaiweka misingi ya dunia.Mimi nawaambieni enyi watu wa Siyoni:‘Nyinyi ni watu wangu.’”

17. Amka ewe Yerusalemu!Amka usimame wima!Mwenyezi-Mungu amekunywesha kikombe cha ghadhabu yake,nawe umeinywa mpaka tone la mwisho,mpaka ukayumbayumba.

Kusoma sura kamili Isaya 51