Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 51:16-23 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Nimeyaweka maneno yangu mdomoni mwako;nimekuficha katika kivuli cha mkono wangu.Mimi nilizitandaza mbingu,nikaiweka misingi ya dunia.Mimi nawaambieni enyi watu wa Siyoni:‘Nyinyi ni watu wangu.’”

17. Amka ewe Yerusalemu!Amka usimame wima!Mwenyezi-Mungu amekunywesha kikombe cha ghadhabu yake,nawe umeinywa mpaka tone la mwisho,mpaka ukayumbayumba.

18. Kati ya watoto wote uliowazaahakuna yeyote wa kukuongoza.Hakuna hata mmoja wa kukushika mkonokati ya watoto wote uliowalea.

19. Majanga haya mawili yamekupata:Uharibifu na maangamizi; njaa na mauaji.Nani atakayekuonea huruma?Nani atakayekufariji?

20. Watoto wako wamezirai,wamelala pembeni mwa kila barabara,wako kama paa aliyenaswa wavuni.Wamepatwa na ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu,wamepatwa na adhabu ya Mungu wako.

21. Basi, sikiliza ewe Yerusalemu unayeteseka;sikiliza wewe uliyelewa, lakini sio kwa divai.

22. Bwana, Mwenyezi-Mungu, Mungu wako,awateteaye watu wake, asema hivi:“Nimekuondolea kikombe cha kuyumbisha,hutakunywa tena kikombe cha ghadhabu yangu.

23. Nitawanywesha watesi wako kikombe hichowaliokuambia ulale chini wapite juu yako;wakaufanya mgongo wako kama ardhi,kama barabara yao ya kupitia.”

Kusoma sura kamili Isaya 51