Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 50:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kama nimempa talaka mama yako Yerusalemu,hati ya talaka iko wapi?Au kama niliwauza utumwani,yuko wapi basi, huyo niliyemwuzia?Kumbukeni mliuzwa utumwani kwa maovu yenu,mama yenu alifukuzwa kwa makosa yenu.

2. “Nilipokuja kwa nini sikukuta mtu?Nilipoita mbona hamkuitikia?Je, mkono wangu ni mfupi nisiweze kuwaokoeni?Je, sina nguvu ya kuwakomboa?Tazama! Kwa kuikemea kidogo bahari hukauka,na mito nikaifanya kuwa jangwa,samaki wake wakafa na kunuka kwa kukosa maji.

3. Mimi hulivika anga giza,na kulivalisha vazi la kuomboleza.”

4. Bwana Mungu amenipa ufasaha wa lugha,niwatie moyo wale waliochoka.Kila asubuhi hunipa hamuya kusikiliza anayotaka kunifunza.

5. Bwana Mungu amenifanya msikivu,nami sikuwa mkaidiwala kugeuka mbali naye.

6. Mgongo wangu niliwaachia walionipiga,mashavu yangu waliozingoa ndevu zangu;walioniaibisha na kunitemea mate,sikujificha mbali nao.

7. Bwana Mungu hunisaidia,kwa hiyo siwezi kufadhaika.Uso wangu nimeukaza kama jiwe;najua kwamba sitaaibishwa.

Kusoma sura kamili Isaya 50