Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 5:24-30 Biblia Habari Njema (BHN)

24. Kwa hiyo, kama moto uteketezavyo nyasi,kama majani yateketeavyo katika mwali wa motondivyo na mizizi yao itakavyooza,na maua yao yatakavyopeperushwa juu kama vumbi.Maana wameiacha sheria ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi,wamedharau neno la yule Mtakatifu wa Israeli.

25. Kwa hiyo hasira ya Mwenyezi-Mungu iliwawakia watu wake,akaunyosha mkono wake dhidi yao, akawachapa,hata milima ikatetemeka,maiti zao zikawa kama takatakakatika barabara za mji.Hata hivyo, hasira yake haikutulia,mkono wake bado ameunyosha kuwaadhibu.

26. Mwenyezi-Mungu analiashiria taifa la mbali;anawapigia mruzi watu kutoka miisho ya dunia;nao waja mbio na kuwasili haraka!

27. Hawachoki wala hawajikwai;hawasinzii wala hawalali;hakuna mshipi wao uliolegeawala kamba ya kiatu iliyokatika.

28. Mishale yao ni mikali sana,pinde zao zimevutwa tayari.Kwato za farasi wao ni ngumu kama mawe;mwendo wa magurudumu ya magari ni kimbunga.

29. Askari wao wananguruma kama simba;wananguruma kama wanasimbaambao wamekamata mawindo yaona kuwapeleka mahali mbaliambapo hakuna awezaye kuwanyanganya.

30. Siku hiyo, watanguruma juu ya Israelikama mvumo wa bahari iliyochafuka.Atakayeiangalia nchi kavuataona giza tupu na dhiki,mwanga utafunikwa na mawingu.

Kusoma sura kamili Isaya 5